Home Yanga SC MWAMBUSI: KOCHA WA MAKIPA AMEPATIKANA

MWAMBUSI: KOCHA WA MAKIPA AMEPATIKANA


KOCHA wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa tayari wameshampata kocha wa makipa wa timu hiyo ambaye ataungana  na kambi hivi karibuni tayari kwa maandalizi ya michezo inayofuata ya Yanga.

Kwa sasa ndani ya Yanga, kocha ambaye anasimamia mazoezi ya makipa ni kocha wa viungo wa timu hiyo Edem Mortotis.

Yanga imekuwa bila kocha wa makipa kutokana na hivi karibuni uongozi wa timu hiyo kuvunja benchi la ufundi likijumisha pamoja na aliyekuwa kocha mkuu wa makipa Vladimr Niyonkuru.

Akizungumzia ishu hiyo Mwambusi amesema: “Timu ilikuwa inamuhitaji zaidi kocha wa makipa na ndio maana lilikuwa ni jambo la haraka,tayari kocha ameshapatikana na atajiunga na kambi ya hivi karibuni,”

SOMA NA HII  MAYELE HAONEKANI KAMBINI...APIGWA CHINI YANGA...ISHU NZIMA IKO HIVI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here