Home Simba SC NYOTA WANNE SIMBA WAWEKA REKODI BONGO

NYOTA WANNE SIMBA WAWEKA REKODI BONGO


NAHODHA wa Simba, John Bocco anaongoza kwa wazawa wenye mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa nayo tisa kibindoni pia ana pasi mbili za mabao.

Namba hiyo ya Bocco inakwenda sambamba na mshikaji wake Meddie Kagere ambaye yeye pia ametupia jumla ya mabao tisa.

Kagere ni mshambuliajiambaye anapambana kuweza kurejesha kiatu chake cha ufungaji bora ambacho alisepa nacho msimu wa 2019/20.

Wakati mabingwa hao watetezi wakiwa ni namba moja kwa upande wa kutupia mabao mengi wakiwa nayo 45 pia watengeneza mipango namba moja wanatokea Simba wakiwa na pasi tisa.

Luis Miquissone mwenye mabao matatu ana pasi tisa za mabao sawa na Clatous Chama mwenye mabao sita na ana pasi tisa za mabao.

Didier Gomes Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ushindi ndani ya uwanja unamtegemea kila mchezaji hivyo kila mmoja ana kazi ya kupambana kufanya vizuri.

“Kila mchezaji ana jukumu la kupambana ndani ya uwanja ili kuipa timu ushindi, imani yangu ni kwamba kwa sasa kila mchezaji analitambua hilo na tutapambana kufanya vizuri,”.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA YANGA WAKITAMBA SANA...SAKHO KWA HASIRA KANG'ATA MENO..KISHA AKASEMA HAYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here