Home Simba SC ORODHA YA MASTAA TISA NDANI YA SIMBA AMBAO MIKATABA YAO ITAFIKA UKINGONI

ORODHA YA MASTAA TISA NDANI YA SIMBA AMBAO MIKATABA YAO ITAFIKA UKINGONI


 IKIWA kesho inatarajiwa kuanza safari kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Al Merrikh, nyota wake 9 mikataba yao inatarajiwa kumeguka msimu utakapoisha.

Simba chini ya Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu, inakazi ya kusaka ushindi ndani ya kundi A ambapo kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi sita baada ya kukusanya pointi hizo kwenye mechi zake mbili.

Hawa hapa nyota hao ambao mikataba yao inaweza kumeguka msimu ukikamilika ndani ya ligi 2020/21:-  Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein `Tshabalala’ kiungo mkabaji Jonas Mkude nahodha John Bocco.

Kipa namba mbili, Beno Kakolanya kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib beki wa pembeni Shomari Kapombe na Gadiel Michael.

Pia kiungo Francis Kahata wengi wanapenda kumuita kijiko na kiungo mshambuliaji Miraji Athumani.

Kuhusu wachezaji kundoka ndani ya Simba, hivi karibuni Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema kuwa mpango wa Simba ni kuwa na wachezaji makini na haitaweza kumuachia mchezaji yeyote ambaye anatakiwa ndani ya kikosi hicho kinachotetea taji la Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.


SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA POLISI TZ LEO...SIMBA WAWEKA MATUMAINI KWA WAZAMBIA WAKE...