Home Ligi Kuu POLISI TANZANIA YAIPIGIA HESABU NAFASI YA KMC

POLISI TANZANIA YAIPIGIA HESABU NAFASI YA KMC


MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kumaliza ndani ya tano bora kwa msimu wa 2020/21.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 23 imekusanya pointi 30 ipo nafasi ya 9 na kinara ni Yanga mwenye pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 huku nafasi ya tano ikiwa mikononi mwa KMC yenye pointi 35.

Akizungumza na Spoti Xtra, Malale alisema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kumaliza ndani ya tano bora jambo ambalo linawezekana.

“Bado tuna mechi za kucheza na hesabu zetu ni kuona kwamba tunamaliza kwenye msimamo tukiwa ndani ya tano bora ili tupate nguvu ya kuanza vizuri msimu ujao.

“Kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wangu mwanzo mwa msimu ilifanya tuanze kwa kusuasua ila kwa sasa hawa ambao wamekuja wameipa nguvu timu na tunazidi kupambana kupata matokeo,” alisema Malale.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAINYOOSHA TANZANIA PRISONS, AZAM V KAGERA YAWEKA REKODI