Home Yanga SC SIBOMANA AIFIKISHA YANGA FIFA KISA MADAI YA MKWANJA WAKE

SIBOMANA AIFIKISHA YANGA FIFA KISA MADAI YA MKWANJA WAKE

 


ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Yanga, Patrick Sibomana amesema kuwa tayari amewasilisha malalamiko yake mbele ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kuhusu madai yake dhidi ya Yanga na kuambiwa jambo hilo linafanyiwa kazi na atapata majibu ndani ya miezi mitatu hadi minne.

 

Sibomana amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na waajiri wake hao wa zamani kutokana na kuwadai kiasi cha dola 4,000, sawa na shilingi milioni 9.2, ambazo zinatokana na fedha za usajili pamoja na sehemu ya mishahara yake.

 

Pande hizo mbili zimekuwa zikiwasiliana mara kwa mara ili kutafuta suluhu, ambapo nyota huyo aliwapa muda hadi kufikia Machi Mosi na kama wasingefanya, hivyo basi angepeleka malalamiko yake Fifa.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Sibomana alisema: “Ni kweli nimepeleka rasmi malalamiko yangu Fifa kuhusu madai yangu dhidi ya Klabu ya Yanga, hii ni baada ya kushindwa kuwa na muafaka mzuri kuhusu malipo ya fedha zangu, hivyo nimefikisha malalamiko yangu katika eneo ambalo naamini haki itatendeka.

 

“Fifa wameniambia kuwa suala hilo linafanyiwa kazi, na watanipa majibu ndani ya miezi mitatu hadi minne.”


Hivi karibuni kuhusu sakata hilo, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa aliliambia Gazeti la Championi: “Ni kweli tumepokea malalamiko ya Sibomana na tunaendelea kulifanyia kazi suala hilo,” .

SOMA NA HII  MAYELE:- YANGA TUNA KAZI YA KUFANYA...KULE MALI TULISHINDWA ...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here