Home Simba SC SIMBA KAMILI GADO KUIVAA PRISONS LEO KWA MKAPA

SIMBA KAMILI GADO KUIVAA PRISONS LEO KWA MKAPA


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo Machi 10 kina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Tanzania Prisons 1-0 Simba.

Leo itakuwa ni mchezo wa kisasi kwa Simba kusaka ushindi huku Prisons wao wakihitaji kulinda rekodi ya kutofungwa na Simba msimu huu wa 2020/21.

Gomes ameweka wazi kwamba maandalizi yamekamilka na anatambua mchezo utakuwa mgumu ila anahitaji pointi tatu.

“Maandalizi ya kikosi yapo sawa na kila mmoja yupo sawa kwa ajili ya kuona kikosi kinapata pointi tatu hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti,” .

Kwa upande wa Salum Mayanga, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons amesema kuwa wanatambua kutakuwa na ushindani mkubwa ila wanahitaji pointi tatu.

SOMA NA HII  KISA SIMBA KUFUNGWA JANA...MANARA ASHINDWA KUJIZUIA...AIBUKA NA 'KICHAMBO KIPYA MJINI'..