Home Taifa Stars STARS YAPAA KUWAFUATA KENYA, KASEJA AAHIDI MAKUBWA

STARS YAPAA KUWAFUATA KENYA, KASEJA AAHIDI MAKUBWA


KIKOSI cha Taifa Stars kimeanza safari ya kuelekea nchini kwa ajili ya michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya.

Stars inataka kuitumia michezo hiyo hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa Machi 15, na 18 mwaka huu kama sehenu ya maandalizi ya michezo ya kusaka tiketi ya michezo ya kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

Stars chini ya kocha, Kim Poulsen ilianza kambi rasmi siku ya Jumatatu iliyopita katika uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumzia maandalizi yao mchezaji Mwandamizi, Juma Kaseja amesema: “Kikosi kimekuwa na wasaa mzuri wa mazoezi ya kujiandaa na michezo yetu dhidi ya Kenya na ile ya kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON.

“Tunajua mbele ya Kenya haitakuwa michezo rahisi kutokana na ukweli kwamba tunajuana vizuri, lakini kutokana na ari niliyoiona kwa wachezaji naamini tutafanya kitu kizuri,”

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUPEWA NDEGE NA SERIKALI..TAIFA STARS YAPEWA JUKUMU HILI LINGINE...