Home Ligi Kuu WAAMUZI WATAKIWA KUTIMIZA MAJUKUMU KWA WELEDI

WAAMUZI WATAKIWA KUTIMIZA MAJUKUMU KWA WELEDI


SUD Abdi Mohamed, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania amesema kwamba ni jukumu la kila mwamuzi kutumia weledi wake wote kazi katika kutimiza majukumu yake.

Kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kumekuwa na matukio ya wachezaji kuonekana wakiwalalamikia waamuzi kutokana na kutoridhishwa na maamuzi yao.

Pia wachezaji nao wamekuwa wakifanya makosa ambayo yanawafanya waamuzi wawaadhibu kwa kuwaonyesha kadi na wakati mwingine kwa kuzungumza nao ili wasiweze kurudia makosa hayo.

Mohamed amesema kuwa wamekuwa wakiwapa mafunzo waamuzi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa weledi jambo ambalo wanatakiwa kulifanya muda wote.

“Waamuzi wote wamekuwa wakipewa mafunzo kila wakati hasa pale ligi inapoanza na tumekuwa tukikumbushana umuhimu wa kutimiza majukumu kwa kufuata sheria na ikiwa watafanya hivyo wataepuka makosa ambayo yanatokea.

“Ikiwa wakikosea kuna kamati maalumu ambayo huwa inapitia ripoti pamoja na yale malalamiko kisha maamuzi huwa yanatolewa hivyo jambo la msingi kwao ni kutimiza wajibu,” amesema.

SOMA NA HII  VITA YA KUSHUKA DARAJA SI MCHEZO, CHEKI RATIBA KAMILI ILIVYO