Home Azam FC WAWILI WA AZAM FC KUIKOSA MWADUI FC LEO

WAWILI WA AZAM FC KUIKOSA MWADUI FC LEO


 NICO Wadada, beki wa kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo atakosekana kwenye kikosi kitakachomenyana na Mwadui FC, Uwanja wa Mwadui Complex.

Wadada aliumia kwenye mazoezi wakati timu hiyo ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

Mchezo huo ubao wa Kaitaba baada ya dakika 90 ulisoma Kagera Sugar 1-2 Azam FC ambapo nyota huyo alikosekana.

Pia Abdalah Kheri, ‘Sebo’ yeye aliumia kwenye mchezo huo na hakuweza kuyeyusha dakika zote 90.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, amesema kuwa maandalizi yameshakamilika kwa asilimia 100 ni suala la kusubiri wakati ndani ya uwanja.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Azam Complex, ubao ulisoma Azam FC 3-0 Mwadui FC hivyo leo utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa Mwadui huku Azam FC wakihitaji kulinda rekodi zao.

SOMA NA HII  AZAM FC WAENDELEA KUFANYA MAKUBWA...WASHUSHA 'KOCHA JIPYA' LA MPIRA...NI BALAA...