Home Yanga SC YANGA KAZI INAENDELEA, WAPEWA PROGRAM MAALUMU KUWAREJESHA KWENYE UBORA

YANGA KAZI INAENDELEA, WAPEWA PROGRAM MAALUMU KUWAREJESHA KWENYE UBORA


 KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi, ameanza kwa spidi ya aina yake katika kikosi hicho akiweka program ya kufanya mazoezi mara mbili kwa siku ikiwa ni maalum kujenga utimamu wa mwili.

 

Kocha huyo ameweka program hizo kwa mastaa wake ambazo alianza kuzifanyia kazi tangu Jumatatu ya wiki hii ikiwa ni baada ya kuona mapungufu ndani ya kikosi hicho.

 

Mwambusi alikabidhiwa mikoba ya kuinoa Yanga kwa mara nyingine baada ya uongozi wa timu hiyo kumvunjia mkataba aliyekuwa kocha wake, Cedric Kaze.

 

“Kwa siku hizi programu ambayo tunaifanya ni kufanya mazoezi mara mbili kwa siku, kisha Ijumaa tutafanya mara moja.

 

“Programu hii imelenga kurejesha utimamu wa mwili kwa wachezaji lakini pia kujenga uwezo wa pamoja kama timu kutokana na mapungufu ambayo yalionekana kwenye kikosi.

 

“Tunajiandaa kupambana na yeyote yule atakayekuja mbele yetu, kwani siku zote kocha unapoandaa timu huwa hatutazamii timu moja tu, natoa mazoezi ili ligi itakapoanza tuwe na uhakika wa kupata pointi tatu mbele ya yeyote.

 

“Hadi sasa nina imani kubwa endapo tutapata muda mrefu huu wa kuwa pamoja hakika tutakuwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mzunguko ujao,” alisema Mwambusi.

SOMA NA HII  YANGA KUIFUATA JKT TANZANIA KWA TAHADHARI LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here