Home Yanga SC YANGA: TUKO TAYARI KUWAVAA COASTAL

YANGA: TUKO TAYARI KUWAVAA COASTAL


KIKOSI cha klabu ya Yanga leo kimefanya mazoezi yao ya mwisho kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union huku wakitamba kufanya vizuri katika mchezo huo.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Mkwakwani, jijini Tanga majira ya saa 10 kamili jioni.

Yanga wametamba kuwa, ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kengold, katika michuano ya kombe la Shirikisho umezidi kuamsha ari ya kushinda mchezo wa kesho.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amewaomba Wanayanga kujitokeza kwa wingi, ili kuwapa sapoti wachezaji wa kikosi hicho.

“Kikosi chetu kimekamilisha mazoezi ya mwisho leo kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union.

“Ni wazi ushindi tulioupata katika mchezo uliopita dhidi ya Kengold kwenye michuano ya kombe la FA, umezidi kutupa ari ya kufanya vizuri kwenye mchezo huu,”

SOMA NA HII  UKWELI KUHUSU KIUNGO MPYA WA YANGA HUU HAPA....ISHU YA FEI TOTO YATAJWA TENA..