Home Yanga SC YANGA:COASTAL UNION WATATUKAMIA NDANI YA MKWAKWANI

YANGA:COASTAL UNION WATATUKAMIA NDANI YA MKWAKWANI


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa anaamini wapinzani wao Coastal Union watawakamia ndani ya Uwanja wa Mkwakwani ili kupata matokeo.

Machi 4, Coastal Union inayonolewa na Juma Mgnda itawakaribisha Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga ilishinda mabao 3-0.

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 49 inakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya 13 na pointi zake kibindoni ni 23.

Kaze amesema:”Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu na wapinzani wetu watatukamia ili kupata matokeo chanya hivyo nasi pia tutapambana kufanya vizuri.

“Tunachohitaji ni ushindi hilo lipo wazi na kila mchezaji anatambua kwamba tunahitaji ushindi, kikubwa ni kupata pointi tatu ndani ya uwanja,” amesema.


SOMA NA HII  SIMBA- KESHO YANGA WATASHINDA ...LAKINI....!!!