Home Ligi Kuu BARAZA ATAMBA KUUWASHA MOTO KAGERA SUGAR

BARAZA ATAMBA KUUWASHA MOTO KAGERA SUGAR


KOCHA mkuu mpya wa klabu ya Kagera Sugar, Francis Baraza ametamba kuwa kikosi chake kitafanya vizuri katika michezo ijayo kutokana na programu za mazoezi wanazoendelea kuzifanya.

Baraza alijiunga na Kagera Sugar na kutambulishwa rasmi Machi 17, mwaka huu akitokea kikosi cha klabu ya Biashara United ya mkoani Mara aliyohudumu kwa misimu miwili.

Kocha huyo anatarajia kuiongoza Kagera Sugar kwa mara ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Machi 8, mwaka huu.

Akizungumzia programu za mazoezi ya kikosi chake Baraza alisema: “Nashukuru kwa kupata nafasi ya kukiona kikosi changu na kufanya nao mazoezi kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa.

“Siwezi kusema kuna mapungufu makubwa lakini tunafanya maboresho kidogo ya mbinu kwa kuongezea kile walichokuwanacho na yale machache mapya ya kwangu,”

SOMA NA HII  KOCHA JKT TANZANIA: TUMEFUNGWA MABAO MEPESI NA YANGA