Home kimataifa KIGOGO WA SUPER LEAGUE AKOMAA

KIGOGO WA SUPER LEAGUE AKOMAA


 FLORENTINO Perez, Rais wa Klabu ya Real Madrid amesema kuwa madai ya European Super League kwamba itaua ligi za ndani ya nchi siyo kweli.

Pia Perez ambaye ni rais wa ligi hiyo amesisitiza kuwa ligi hiyo haijafutwa rasmi bali imesimama kwa muda kutokana na timu 6 ambazo zinashiriki Ligi Kuu England kujitoa ila awali zilikubali kushiriki ambapo ni pamoja na Chelsea, Liverpool, Arsenal, Manchester United na Spurs.

Ligi hiyo mpya ambayo ilianzishwa hivi karibuni imekuwa ikipingwa na wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na mashabiki ambapo wameweka wazi kwamba itavuruga utamu ligi pamoja na mashindano mengine.

Kigogo huyo anaamini kuwa inawezekana wamekosea katika kuuelezea mradi huo lakini bado anaamini kwamba ni ligi sahihi kwa kuwa mradi huo ulianzishwa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.

“Ninasikitishwa na nimeangushwa kwa hiki kinachoendelea, tumeufanyia kazi mradi kwa miaka mitatu sasa. Lengo ni kupata fedha katikati ya wiki.

“Katika timu 12 waanzilishi msimu uliopita tulipata hasara ya euro 650 milioni. Msimu huu inaweza kuwa mara mbili au tatu ya hiyo mfumo hiyo ni wazi,”.



SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED YAJIPIGIA CITY NDANI YA LIGI KUU ENGLAND

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here