Home Simba SC KUMBE MO DEWJI ALIWAMALIZA AS VITA MAPEMA TU

KUMBE MO DEWJI ALIWAMALIZA AS VITA MAPEMA TU

MWENYEKITI wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji na viongozi wa Simba kumbe waliimaliza mapema tu mechi ya Simba na AS Vita.

Simba jana iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi uliopigwa katika dimba la Mkapa.

Sasa unaambiwa kuelekea mchezo huo kumbe, boss huyo wa Simba aliomba kukutana na wachezaji wa Simba usiku wa kuamkia jana na kuweka mikakati mizito ya kuwamaliza AS Vita ikiwemo kuwatangazia dau nono iwapo wataibuka na ushindi.

Simba wanaoongoza msimamo wa kundi A la michuano hiyo baada ya kujikusanyia pointi 13  baada ya kucheza michezo mitano. na kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali.

Katika michezo miwili ambayo Simba ilicheza nyumbani katika michuano hiyo mwaka huu kikosi hicho kilifanikiwa kuvuna kiasi cha Shilingi Milioni 600, Milioni 400 kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly na milioni 200 kwenye mchezo dhidi ya Al Merrikh.

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya klabu ya Simba kimesema kuwa bosi huyo wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba alimaliza kila kitu mapema.

β€œMwenyekiti wetu wa bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji β€˜MO’, juzi usiku alikutana na wachezaji wote na kupata chakula cha usiku na kikosi kizima, huku pia akitumia muda huo kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji na kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kuhakikisha tunashinda dhidi ya AS Vita.

β€œNi katika kikao hicho ndipo aliweka wazi kiasi cha fedha ambacho wachezaji na benchi la ufundi wangepata baada ya kushinda mchezo dhidi ya AS Vita.


SOMA NA HII  GOMES AWATAKA WACHEZAJI WAWE MAKINI KWENYE MIPIRA ILIYOKUFA