Home Simba SC MCHEZAJI YANGA : CHAMA, LUIS NI HATARI

MCHEZAJI YANGA : CHAMA, LUIS NI HATARI


ALIYEWAHI kuwa nyota wa klabu ya soka ya Yanga na timu ya Taifa , Taifa Stars Ally Mayay amesema kuwa uwezo mkubwa wanaouonyesha wachezaji Clatous Chama na Luis Miquissone katika kufunga na kutengeneza mabao ni miongoni mwa sababu kubwa zinazoibeba Simba.

Miquissone na Chama wamekuwa katika kiwango cha hali ya juu msimu huu ambapo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika nyota hao wawili wamehusika katika mabao 13 katika michezo tisa waliyocheza.

Chama amefunga mabao manne na kuasisti mara tatu, huku Miquissone yeye akifunga mabao matatu, kaasisti mabao mawili na kutengeneza penalti moja.

Kutokana na uwezo mkubwa wanaouonyesha, nyota hao wawili walichaguliwa kuwa katika kikosi bora cha wiki cha Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia ubora wa nyota hao, Ally Mayay kuhusu uwezo wa nyota hao amesema: “Ni suala lililowazi kwamba Simba kwa sasa wapo katika kiwango bora kabisa, na hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kuendana kwa falsafa ya timu hiyo na aina ya wachezaji walionao.

“Falsafa ya Simba kwa miaka yote ni kucheza soka la kumiliki mpira na nadhani kwa sasa wamefanikiwa zaidi katika hilo kwa kuwa wana wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kama ilivyo kwa Luis na Chama,”

Licha ya kuwa na mchezo mmoja mkononi Simba tayari imefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, baada ya kujikusanyia pointi 13 katika michezo mitano waliyocheza mpaka sasa.

SOMA NA HII  NYOTA WENGINE SIMBA AMBAO MIKATABA YAO INAKARABIA KUMEGUKA ORODHA HII HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here