Home Simba SC MORRISON AWAFANYIA MAZOEZI MAALUMU MABOSI WAKE WA ZAMANI

MORRISON AWAFANYIA MAZOEZI MAALUMU MABOSI WAKE WA ZAMANI


ZIKIWA zimebaki takribani siku nane kabla ya Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga, Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amesema atakuwa akifanya mazoezi maalum kwa ajili ya mchezo huo.

 

Morrison ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Yanga, kama akicheza mechi hii, itakuwa ni mara ya kwanza kucheza dhidi ya Yanga baada ya ile ya kwanza iliyochezwa Novemba 7, 2020, kukosekana.

 

Tayari Morrison amecheza Kariakoo Dabi mbili akiwa Yanga ambapo ya kwanza alifunga bao pekee lililoipa Yanga ushindi wa 1-0 kwenye Ligi Kuu Bara, kabla ya ile ya pili Simba kushinda 4-1 ndani ya Kombe la FA.

 

Mei 8, mwaka huu, Simba itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Morrison amesema kuwa: “Haina haja ya mimi kuwazungumzia Yanga kwani sioni maana ya kuizungumzia maana mimi mwenyewe naonekana kama Simba, kwa hiyo tusubirie siku yenyewe.

 

“Nimejipanga na mazoezi maalum kuelekea mchezo huo kwani ni mchezo mkubwa na wa kwanza kwangu nikiwa Simba.”



SOMA NA HII  HENOCK INONGA BAKA ATAJWA BEKI BORA MSIMU HUU...AMIMINIWA MISIFA KAMA YOTE...