Home Azam FC PRINCE DUBE APEWA PROGRAM MAALUMU KURUDI KWENYE UIMARA

PRINCE DUBE APEWA PROGRAM MAALUMU KURUDI KWENYE UIMARA

 


NYOTA wa Azam FC,  Prince Dube baada ya kurejea kwenye uimara wake amepewa program maalumu itakayomfanya awe fiti zaidi.

Ndani ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina, Dube ni kinara wa kutupia akiwa na mabao nane pia ametengeneza jumla ya pasi tano za mabao.

Azam FC ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza jumla ya mechi 24 imekusanya pointi 44 kibindoni.

Ofisa Habari wa Azam FC,  Thabit Zakaria amesema kuwa kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi huku wale waliokuwa wanasumbuliwa na majeruhi wakiwa wamepewa program maalumu.

Dube alikuwa anasumbuliwa na nyama za paja jambo ambalo lilimfanya awe nje kwa muda ila kwa sasa tayari ameshaanza mazoezi.

Mchezo wake ujao Azam FC itamenyana na Mtibwa Sugar ambayo iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Uwanja wa Jamhuri,Morogoro.


SOMA NA HII  ALIYEMTULIZA KAGERE ATOA KAULI YA KIBABE