Home Simba SC SIMBA SC WATUMIA BILIONI 1 KUPATA USHINDI MECHI ZA CAF

SIMBA SC WATUMIA BILIONI 1 KUPATA USHINDI MECHI ZA CAF


 IMEFAHAMIKA kuwa Simba imetumia kitita cha shilingi bilioni moja katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Simba tayari imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika baada ya kuwafunga AS Vita mabao 4-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Aprili 3.

 

Timu hiyo imefuzu hatua hiyo ya makundi ikiwa inaongoza katika msimamo Kundi A, ikiwa na pointi 13 ikiwa imebakisha mchezo mmoja pekee dhidi ya Al Ahly utakaopigwa leo Ijumaa huko Cairo, Misri.


Taarifa zimeeleza kuwa Simba imetumia Sh 1Bil iliyotumika kwa ajili ya kuwapa bonasi wachezaji na benchi la ufundi.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa bonasi hiyo imetumika kwa ajili ya kuwaongezea morali na hali ya kujituma kwa wachezaji wake ili kufanikisha ushindi.

Aliongeza kuwa bonasi hiyo imehusisha michezo ya kimataifa pekee tofauti na Ligi Kuu Bara ambayo huko ipo bajeti nyingine inayojitegemea.

 

“Michuano ya kimataifa ina umuhimu wake, hivyo imetengwa bajeti maalum kwa ajili ya bonasi ya wachezaji wetu ambayo imetengwa katika makundi mawili.

 

“Makundi hayo kama timu ikifanikiwa ushindi kuna kiwango cha pesa ambacho wachezaji na benchi la ufundi, endapo timu ikipata ushindi na sare lakini timu ikifungwa hawapati bonasi.

 

“Hivyo hadi timu yetu inafanikiwa kufuzu robo fainali tumetumia kiwango cha Sh 1Bil kama sehemu ya bonasi kwa wachezaji na benchi la ufundi na hiyo ni katika kuwaongezea morali na hali ya kujituma,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mshauri wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Crescentius Magori hivi karibuni alizungumzia hilo la posho la wachezaji na kusema kuwa: “Hilo la posho lipo katika mikataba yetu kati ya wachezaji na uongozi.

 

“Hivyo wachezaji wetu tumewawekea utaratibu wa kuwapatia posho katika kuongeza morali ya ushindi pale wanapoipatia timu matokeo mazuri ya ushindi, hivyo hilo lipo katika timu yetu.”


SOMA NA HII  KISA MICHUANO YA CAF....MBRAZILI ATIMKA SIMBA...ARUDI KWAO BRAZIL USIKU USIKU..