Home Simba SC SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU MANULA KUSEPA KUELEKA KWA WAARABU

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU MANULA KUSEPA KUELEKA KWA WAARABU


 KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes ameibuka na kutamka kuwa kamwe hatakubali kumuachia kipa wake namba moja Aishi Manula aondoke katika kikosi chake kutokana na ubora wake alionao.

 Hiyo ni baada ya kupata taarifa za kipa huyo kuwaniwa na Al Merrikh ya nchini Sudan ambayo nayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, msimu huu.

 

Gomes amesema kuwa amezisikia taarifa za kipa wake kuhitajika na Merrikh ambazo kwake hazimtishi akiamini Manula hatakwenda huko na badala yake ataendelea kubakia kukipiga Simba.


Mfaransa huyo amesema kuwa ni ngumu kwake kumuachia Manula kwa hivi sasa kutokana na uimara, kiwango bora alichonacho hivyo atahakikisha anapambana kuishawishi Bodi ya Wakurugenzi ya Simba iliyo chini ya mwenyekiti wake Mohammed Dewji ‘Mo’ imbakize Simba.

 

Gomes anapata jeuri ya kipa huyo kubakia Simba kutokana na timu hiyo aliyokuwa anaifundisha kutokuwa na uwezo wa kifedha kumsajili baada ya kuyumba kiuchumi.

 

“Mimi nilikuwepo Merrikh kabla ya kuja Simba, hivyo ninaifahamu vizuri timu hiyo akiwemo rais wake hivyo ni ngumu kumsajili Manula.

 

“Timu hiyo ninafahamu imeyumba kiuchumi hivi sasa hivyo hawana fedha ya kumsajili na kingine hata kama wangekuwa na fedha kiasi gani nisingeweza kumruhusu kuondoka Simba na hiyo ni kutokana na ubora wake.

 

“Siyo Merrikh hata klabu nyingine yoyote asingeondoka, lipo wazi Manula yupo katika kiwango bora zaidi, ni kipa anayejua majukumu yake vizuri.


“Nimepata taarifa za kuwa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo nitazungumza na viongozi kwa ajili ya kumuongezea mkataba mpya ili aendelee kubakia hapa Simba,” amesema Gomes.


Chanzo:Championi


SOMA NA HII  TSHABALALA - YA AFRIKA KUSINI YASHAPITA..KILICHOPO MBELE YETU NI HALALI YETU..HATUNA KUREMBA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here