Home Yanga SC UONGOZI WA YANGA KUKETI NA NTIBANZOKIZA ILI KUJUA TATIZO LIPO WAPI

UONGOZI WA YANGA KUKETI NA NTIBANZOKIZA ILI KUJUA TATIZO LIPO WAPI


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utakaa na mchezaji wao Said Ntobanzokiza ili kujua ni kipi ambacho kinamsumbua kutokana na kitendo chake cha kuonekana amekasirika baada ya kufunga bao, Aprili 20 mbele ya Gwambina FC.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa nyota huyo hakupenda kuanzia benchi kwa kuwa anaamini kwaba ana uwezo mkubwa wa kucheza jambo ambalo limekuwa likiwakasirisha wachezaji wengine.

 Wakati Yanga ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Gwambina, Ntibanzokiza alianzia benchi na aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Tuisila Kisinda ambaye aliumia.

Mshauri wa Yanga kuelekea kwenye masuala ya mabadiliko, Senzo Mbatha amesema kuwa kwa kitendo ambacho amekifanya ni lazima wazungumze naye ili kujua tatizo.

“Ikiwa mchezaji amefunga ameshindwa kushangilia hiyo inatokea kwenye mchezo kwani kila kitu kinawezekana na muda mwingine inategemea mazingira hivyo sio jambo la kuhoji sana.

“Lakini kwa kuwa imekuwa hivyo na imetokea lazima tuzungumze na mchezaji ili tujue nini ambacho kinamsumbua na tukijua nina amini kwamba tutayamaliza ila ninachojua mimi hakuna tatizo,” amesema.

SOMA NA HII  MABADILIKO YANGA YAANZA KUFANYA KAZI...UCHAGUZI MKUU WAITWA FASTA...RAIS KUONGOZA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here