Home Azam FC AZAM FC V KMC NI SAA 1:00 USIKU, MUDA WABADILISHWA

AZAM FC V KMC NI SAA 1:00 USIKU, MUDA WABADILISHWA


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC dhidi ya KMC utachezwa saa 1:00 usiku badala ya saa 10:00 jioni.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa muda wa mchezo huo umebadilishwa tofauti na awali.

Mwagala amesema:”Mechi yetu ya KMC dhidi ya Azam FC umebadilishwa muda kutoka saa 16:00, (10:00) jioni tena ni saa 19:00, (1:00) usiku, Uwanja wa Chamazi. Nawatakia sikukuu njema,”.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma KMC 1-0 Azam FC hivyo leo utakuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu.
Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya 5 na pointi zake 41 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 54,
SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA AZAM...FEI TOTO AFUNGUKA ISHU YAKE NA RAIS SAMIA...AITAJA YANGA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here