Home FA Cup AZAM FC YAWASILI MWANZA KUWAFUATA RHINO RANGERS

AZAM FC YAWASILI MWANZA KUWAFUATA RHINO RANGERS

 


KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Geroge Lwandamina kimewasili Mwanza leo Mei 24 kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wao Rhino Rangers, Shinyanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.


Mshindi wa mchezo huo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba v Dodoma Jiji unaoatrajiwa kuchezwa Mei 25, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa Rhino Rangers v Azam FC unatarajiwa kuchezwa Jumatano, Mei 26, Uwanja wa Kambarage,  saa 10:00 jioni.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanaamini watafanya vizuri ili kutimiza lengo lao la kutwaa taji hilo.

“Kikosi kwa sasa kimefika Mwanza na baada ya hapo tutaunganisha safari kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Rhino Rangers.

“Wachezaji 23 waliondoka na Shirika la ndege la Air Tanzania kwa ajili ya kucheza na Rhino Rangers na timu itafika leo Shinyanga.

“Mchezo huu ni muhimu kwetu na tunahitaji kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa na namna pekee ya kufanya hivyo ni kushinda mechi zetu za Kombe la Shirikisho,” .

SOMA NA HII  SIMBA KUWAPA MKWANJA WACHEZAJI WA DODOMA JIJI