IPO wazi kuwa kwa sasa uwekezaji katika ulimwengu wa mpira unazidi kutanua wigo ambapo wengi wanapenda kuwekeza na kuona matokeo ambayo yatakuwa mazuri.
Azam Media Limited imeshinda zabuni ya haki za matangazo ya urushaji wa mechi za Ligi Kuu Tanzania bara wenye thamani ya shilingi Bilioni 225.6.
Kiasi hicho ni kikubwa kuwahi kutolewa kwa udhamini wa michezo nchini Tanzania na hata nchi jirani za Afrika Mashariki na Kati.
Kwa mujibu wa mkataba wa miaka 10 uliosainiwa jijini Dar es Salaam, asilimia 67 ya pesa hizo itakwenda moja kwa moja kwa timu ambazo zinashiriki ligi hiyo.
Azam TV pia itakuwa ikitoa zawadi (bonus) kwa Bingwa wa Ligi Kuu Tsh milioni 500, timu zinazofuata katika msimamo mpaka nafasi ya 16 zitakuwa zikinufaika pia.
Serikali itanufaika kwa kupata shilingi bilioni 34.4 zikiwa ni ni kodi ya ongezeko la thamani VAT.