Home Ligi Kuu BREAKING: MAPILATO WA SIMBA V YANGA HAWA HAPA

BREAKING: MAPILATO WA SIMBA V YANGA HAWA HAPA


 BREAKING: KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga, Mei 8, Shirikisho la Soka Tanzania,  (TFF) limetoa orodha ya waamuzi watakaosimamia mchezo huo.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili kwa watani hawa kukutana ambapo ule wa awali walipokutana Uwanja wa Mkapa, Novemba 7 ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imemtaja Emmanuel Mwandembwa kutoka Arusha kuwa mwamuzi wa kati.

Frank Komba wa Dar kuwa mwamuzi msaidizi namba moja.

Hamdan Said kutoka Mtwara kuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.

Na Ramadhan Kayoko kutoka Dar kuwa mwamuzi wa akiba.


SOMA NA HII  TIMU ZA BONGO ZATAKIWA KUMUENZI MAGUFULI KWA VITENDO