Home Simba SC CLATOUS CHAMA APEWA TUZO KWA MWEZI APRILI

CLATOUS CHAMA APEWA TUZO KWA MWEZI APRILI


 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ameibuka kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Mashabiki wa Mwezi Aprili.

Tuzo hiyo inayodhaminiwa na Emirate Aluminium imeanza hivi karibuni kwa lengo la kuwaongezea morali wachezaji wa timu hiyo kufanya vizuri.

Mchezaji wa kwanza kusepa na tuzo hiyo alikuwa na kiungo Luis Miquissone na wa pili alikuwa ni beki Joash Onyango.

Tuzo ya Aprili ambapo Chama alikuwa akipambania na Aishi Manula pamoja na Shomari Kapombe inakuwa ya tatu kutolewa.

Kupitia ukurasa rasmi wa Istagram wa Simba wamemtangaza Chama kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwezi Aprili.

Kiungo huyo amekuwa bora ndani ya uwanja pale anapoamua kwa kuwa wakati mwingine amekuwa akilalamikiwa kucheza chini ya kiwango.

Ndani ya ligi amefunga mabao 7 na kutoa jumla ya pasi 13 akiwa ni kinara kwa upande wa watengeneza mipango msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  KIZAAZAA CHA MZAMIRU YASIN KWENYE DABI, ROBERTINHO ALISEMA HIVI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here