Home FA Cup DODOMA JIJI: TUMEFUNGWA NA TIMU BORA

DODOMA JIJI: TUMEFUNGWA NA TIMU BORA


MBWANA Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa alipoteza mbele ya timu bora katika Kombe la Shirikisho licha ya wachezaji wake kupambana kusaka ushindi.


Jana, ubao wa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ulisoma Simba 3-0 Dodoma Jiji ilikuwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.


Watupiaji kwa Simba alikuwa ni John Bocco aliyetupia mabao mawili na Meddie Kagere alitupia bao moja na kuifanya Simba kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho. 


Akizungumza na Saleh Jembe,  Makata amesema kuwa walikuwa wanahitaji ushindi ila ugumu ilikuwa katika kumaliza nafasi ambazo wamezitengeneza.


“Ulikuwa ni mchezo mgumu na wachezaji walipambana kusaka ushindi ila haikuwa rahisi hasa ukizingatia kwamba wapinzani wetu walikuwa imara katika kutengeneza nafasi na kuzitumia pia ni timu bora.


“Hakuna namna kila mmoja anajua kwamba Simba imetoka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo ni timu imara nasi tumefungwa na timu bora. Tunachokifanya ni kuzidi kujifunza zaidi,” amesema. 


Simba hatua ya nusu fainali itakutana na Azam FC ambayo ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers,  Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

SOMA NA HII  YANGA YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, KUISUBIRI SIMBA V AZAM FAINALI