Home kimataifa FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA MASHABIKI KUISHUHUDIA

FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA MASHABIKI KUISHUHUDIA


 KESHO Mei 29, Uwanja wa Estadio do Dragao, Ureno inatarajiwa kuchezwa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Chelsea na Manchester United ambapo zote zinatoka England.

Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel ilitinga hatua hiyo baada ya kushinda nusu fainali kwa mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid huku City ikishinda mbele ya PSG kwa mabao 4-1.

Inakuwa ni fainali ya tatu kwa Chelsea ambapo zilizopita ilishinda moja na kufungwa moja na unatarajiwa kuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zinahitaji kusepa na taji hilo.

Kwenye mchezo wa kesho jumla ya mashabiki 16,500 wataruhusiwa kushuhudia mchezo huo wakiwa ndani ya uwanja ambapo habari zinaeleza kuwa mashabiki wengi wamefunga safari ili kuweza kushuhudia mchezo huo.

SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED WAPO TAYARI KUMSIKILIZA de GEA