Home Yanga SC LICHA YA KUONDOKA..,YANGA WATAKA MILIONI 480 KWA CARLINHOS

LICHA YA KUONDOKA..,YANGA WATAKA MILIONI 480 KWA CARLINHOS

 


KIUNGO wa ushambuliaji wa Yanga, Carlos Sternio Fernandes ‘Carlinhos’ leo amesepa nchini kurejea kwao Angola baada ya kumalizana na uongozi wa klabu hiyo kwa kusitisha mkataba wake.

Uongozi wa Yanga umethibitisha kusitisha mkataba na mchezaji huyo baada ya majadiliano na kwa kuzingatia maslahi mapana ya pande zote.

Inaelezwa pia amekuwa na kawaida ya kuomba kuondoka katika klabu hiyo baada ya kushindwa kuzoea mazingira ya hapa nchini.

Mmoja wa vigogo wa klabu hiyo amesema mchezaji huyo awali alishapeleka barua ya kuomba kuondoka mara mbili, lakini wiki iliyopita alipopeleka ikiwa ni mara ya tatu, mabosi wa Yanga wameona isiwe tabu.

“Leo Jumatatu kama taratibu za ndege zitaenda sawa basi ataondoka nchini na kurejea kwao, amekuwa na kawaida ya visingizio mara kwa mara kuhusu mazingira ya nchini, mwisho sasa viongozi wamechoka wameona bora aondoke.”

Kigogo huyo aliongeza kusema, “Kuna muda alikuwa anasingiza hawezi kukaa mbali na mkewe lakini bado hakuacha vituko vyake kwahiyo kama viongozi tumeona tumalizane naye vizuri.”

Mchezaji huyo licha ya kusajiliwa kwa mbwembwe hajawa sehemu ya kikosi cha kwanza mara kwa mara kutokana na kusumbuliwa na majeraha mfululizo.

Inaelezwa pia mabosi wa Yanga ni kama wameshtuka kwamba mchezaji huyo anaweza kurejea nchini na wakaamua kuweka baadhi ya vipengele vigumu kwa timu nchini itakayotaka kumsajili katika misimu minne ijayo kuanzia sasa basi nao watafaidika na kiasi fulani cha pesa.

Yanga wameweka kipengele cha fidia ya dola 200,000 (Sh.480 milioni) kama atarejea nchini kujiunga na klabu nyingine ndani ya kipindi cha miaka minne.

Kufikia wakati huo, Carlinhos atakuwa na umri wa miaka 30. Muangola huyo sasa ana miaka 26.

Carlinhos aliandika historia kwa kupokewa na umati mkubwa wakati akiwasili nchini na kuweka katika gari la wazi lililofuatana na msururu wa magari yaliyomtembeza kutoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hadi yalipo Makao Makuu ya Yanga, Mtaa wa Jangwani na alitokwa na machozi akisema hakuwahi kupokewa namna hiyo.

SOMA NA HII  KISA MASHABIKI KULALAMIKA SANA KUHUSU UWEZO WA NABI...YANGA WAFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU...