Home news MAJOGORO:TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO MECHI ZILIZOBAKI

MAJOGORO:TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO MECHI ZILIZOBAKI


 NYOTA wa kikosi cha Mtibwa Sugar,Baraka Majogoro amesema kuwa watapamba akupata matokeo kwenye mechi zao zote zilizobaki ili kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara.

Chini ya Kocha Mkuu, Mohamed Badru ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 30 na imebakiwa na mechi nne kukamilisha mzunguko wa pili utakaofunga msimu wa 2020/21 mazima.


Akizungumza na Saleh Jembe, Majogoro amesema kuwa ushindani msimu huu ni mkubwa na kila timu ina presha ya kupata matokeo jambo ambalo linawafanya nao wapambane kwa hali na mali.

“Kweli hatupo katika nafasi nzuri hasa ukizingatia kwamba pointi tulizo nazo pamoja na nafasi kwetu sio nzuri ambacho tutakifanya ni kupambana kushinda mechi zetu zote zilizobaki na inawezekana kikubwa mashabiki wazidi kutupa sapoti.

“Ushindani ni mkubwa nasi tunapambana kupata pointi tatu kwa sasa hasa ukizingatia tupo kwenye lala salama na kila timu inahitaji pointi tatu,” amesema. Majogoro.

Mechi za Mtibwa Sugar ambazo zimebaki ni dhidi ya Mwadui FC, KMC, Dodoma Jiji na kigongo chao kingine ni dhidi ya JKT Tanzania.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LEO...SAKHO AJIPA KIAPO KIPYA SIMBA..AFICHUA YA SAIDO NTIBAZONKIZA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here