Home epl MANCHESTER UNITED INAHITAJI KUONGEZA WATATU, WENGINE KUONDOKA

MANCHESTER UNITED INAHITAJI KUONGEZA WATATU, WENGINE KUONDOKA


 OLE Gunnar Solskjaer , Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa anahitaji kuongeza nyota wapya watatu ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.

Kocha huyo ambaye msimu huu alikuwa katika ubora wake hasa mechi za ugenini ambapo hawajafungwa mchezo wowte kati ya 19 anahitaji kuongeza nguvu zaidi ili aweze kushindana na mpinzani wake mkubwa Manchester City.

Katika Ligi Kuu England, United imekamilisha msimu kwa kujikusanyia jumla ya pointi 74 ikiwa ni namba mbili huku City ikiwa ni namba moja na pointi zao ni 86.

Mchezo wao wa mwisho kwa msimu United ilishinda jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Wolves.

Kocha huyo amesema:”Kwa sasa tunaangalia kwenye kikosi chetu wachezaji gani watasalia hapa na ambao wanatakiwa kuondoka na pia wale watakaotoka kwenda kupata uzoefu.

“Matumaini yangu kuboresha kikosi changu, wachezaji wawili ama watatu nahitaji ndani ya kikosi changu,”.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUTOA KAFARA YA NG'OMBE ...MISRI WACHEZESHWA 'NDOMBOLO' NA CONGO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here