Home Yanga SC MICHAEL SARPONG APITISHA SAA 4,080 BILA KUFUNGA

MICHAEL SARPONG APITISHA SAA 4,080 BILA KUFUNGA

MICHAEL Sarpong, mshambuliaji wa kikosi cha Yanga raia wa Ghana amepitisha jumla ya siku 170 ambazo ni sawa na saa 4,080  bila kufunga bao kwenye mechi zote za ushindani ikiwa ni zile za Ligi Kuu Bara na Shirikisho.
Kwenye ligi Yanga ina pointi 61 baada ya kucheza mechi 29 na ina mabao 43 amehusika katika mabao 7, alifunga mabao manne, pasi mbili za mabao na alisababisha penalti moja kwenye mchezo dhidi ya KMC, Uwanja wa CCM Kirumba.
Bao lake la kwanza ndani ya ligi alifunga Uwanja wa Mkapa kwenye sare ya kufungana  bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, ni Septemba 6 kisha Oktoba 31 aliwafunga Biashara United, Uwanja wa Karume.
 Novemba 7 aliwafunga Simba ilikuwa ni kwa mkwaju wa penalti na Desemba 6 alifunga akaunti yake ya mabao kwa kuwafunga Ruvu Shooting ilikuwa Uwanja wa Mkapa.
Leo Mei 25 anatarajiwa kuongoza kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC ikiwa ni hatua ya robo fainali.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kambarage majira ya saa 10:00 jioni na mshindi wa jumla atainga hatua ya nusu fainali ambapo atakutana na Biashara United aliyeshinda mbele ya Namungo FC.

SOMA NA HII  ILI KUWAMALIZA KABISA WANIGERIA...MAYELE AWEKEWA MIL 300 CASH MEZANI....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here