Home Tetesi za usajili MTAMBO HUU WA MABAO WAKUBALI KUTUA YANGA

MTAMBO HUU WA MABAO WAKUBALI KUTUA YANGA


 NYOTA wa kikosi cha Dodoma Jiji kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata, Dickson Ambundo amesema kuwa yupo tayari kucheza timu yoyote kwa sasa ikiwa ni pamoja na Yanga ambayo imekuwa ikitajwa kuhitaji saini yake.

Ambundo amekuwa bora kwa takwimu ndani ya uwanja akihusika katika mabao 7 kati ya 27 ambayo yamefungwa na timu hiyo iliyocheza jumla ya mechi 30 ikiwa nafasi ya 8.

Ana pasi 4 za mabao huku akicheka na nyavu mara tatu aliwatungua Tanzania Prisons, Ruvu Shooting na JKT Tanzania. Imekuwa ikielezwa kuwa Yanga wanahitaji kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao na miongoni mwa sekta ambayo wataifanyia kazi ni ile ya kiungo mshambuliaji.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ambudo alisema kuwa hajapata taarifa zozote kuhusu kuhitajika kwake ndani ya Yanga ila ikiwa utaratibu utafuata yeye atacheza sehemu yoyote.

“Mimi kwa sasa ni mchezaji halali wa Dodoma Jiji, ninaweza kucheza popote hata Yanga, lakini sijapata taarifa zozote kuhusu kutakiwa na timu kwa sasa ila ikitokea zikawa zinahitaji saini yangu ni suala la kuzungumza na uongozi pamoja na wale ambao wananisimamia, hao watanipa mimi taarifa,” alisema Ambundo.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA 'WAKIENJOY' SOKA LA PASI SAMBUSA...EL MERRIKH YA SUDAN WAMTAKA TENA NABI..ISHU IKO HIVI...