Home Namungo FC MUUAJI WA YANGA AKUMBWA NA MAJERAHA NAMUNGO

MUUAJI WA YANGA AKUMBWA NA MAJERAHA NAMUNGO


STEVEN Sey, miongoni mwa nyota ambao wamefanikiwa kuifunga Yanga msimu huu ni miongoni mwa wachezaji wanne wa kikosi cha klabu ya soka ya Namungo, ambao wanatarajiwa kuendelea kosekana ndani ya kikosi hiko kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Majeraha.

Namungo hawajawa na wakati mzuri msimu huu ambapo mpaka sasa katika michezo yao mitano mfululizo iliyopita wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee, wakifungwa mchezo mmoja na kutoa suluhu michezo mitatu.

Kutokana na matokeo hayo Namungo wanakamatia nafasi ya 10 kwenye msimamo wakiwa na pointi zao 37 walizokusanya kwenye michezo 27. Wameshinda mechi tisa, wamefungwa mechi nane na kutoa sare michezo 10.

Akizungumzia hali za wachezaji hao Ofisa habari wa kikosi cha Namungo, Kindamba Namlia amesema: “Kikosi chetu kinatarajia kuendelea kuwakosa wachezaji wanne ambao ni Sey, Bigirimana Blaise, Carlos Protas na Haruna Shamte. Sey pamoja na Shamte ni wagonjwa, Bigirimana yeye amekuwa na majeraha ya muda mrefu huku Protas akiwa anarejea kutoka kwenye majeraha.”

SOMA NA HII  KICHUYA AFUNGUKA A-Z KUHUSU DILI LAKE NA SIMBA KWA MSIMU UJAO..."WANANIAMBIA KARIBU NYUMBANI"....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here