Home CAF POZI LA KOCHA MKUU WA KAIZER CHIEFS LAWA GUMZO

POZI LA KOCHA MKUU WA KAIZER CHIEFS LAWA GUMZO


POZI la Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Gavin Hunt alipokuwa kwenye benchi la ufundi jana Mei 15 wakati timu yake ikishinda mchezo wa kwanza mbele ya Simba limezua gumzo kwa wadau wa mpira kutokana na namna ambavyo alifanya huku kila mmoja akitoa maoni yake.


Wapo ambao walisema kuwa hicho ni kicheko cha furaha na wengine wakisema kuwa ni kicheko cha mshangao wa idadi ya mabao aliyoshinda.

Alifanya hivi aliposhuhudia bao la nne kwa timu yake ya Kaizer Chiefs lililopachikwa na Leonardo Castro na ubao wa FNB ulisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ilipoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ina kazi ya kupindua meza katika mchezo wa pili, Uwanja wa Mkapa, Mei 22 ili kuweza kusonga mbele hatua ya nusu fainali.


SOMA NA HII  VIJANA WA IBENGE WAINGIA DOSARI...SAFARI YAO YAKWAMA...LIGI YA MABINGWA AFRIKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here