Home Azam FC SERE BOY ATAMBA KUREJEA KWA KISHINDO

SERE BOY ATAMBA KUREJEA KWA KISHINDO


KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakari “Sure Boy”, amesema kuwa kwa sasa amerudi kwa kasi ya ajabu.

Nyota hyo ameyasema hayo baada ya kutoka kwenye majeraha yaliyomfanya akosekane kwenye mechi mbili dhidi ya Dodoma Jiji ubao ulisoma Dodoma Jiji 2-2 Azam ulichezwa Aprili 22.

Pia Aprili 25, ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Yanga 0-1 Azam FC alikuwa jukwaani akishuhudia mchezo huo.

Kwa sasa Azam ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 54, huku vinara wakiwa Simba wenye alama 61.

Sure Boy amesema kuwa: “Hakuna mchezaji anayependa kuwa majeruhi na mimi niliumia kukaa majeruhi ila nafurahi kwa muda niliokuwa majeruhi timu ilipata ushindi ni jambo zuri. Nimerejea kwa kishindo.”

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza jumla ya mechi 28.


SOMA NA HII  AZAM FC KAZINI TENA LEO KOMBE LA KAGAME