Home Simba SC SIMBA WAKIRI KWAMBA MCHEZO WAO DHIDI YA YANGA UTAKUWA MGUMU

SIMBA WAKIRI KWAMBA MCHEZO WAO DHIDI YA YANGA UTAKUWA MGUMU


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa mchezo wao dhidi ya Yanga utakuwa mgumu ila watapambana kusaka pointi tatu muhimu.

Zimebaki siku tano kwa watani hao wa jadi kukutana Uwanja wa Mkapa, Mei 8 katika mchezo wa ligi kusaka pointi tatu muhimu.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Patrick Rweyemamu, meneja wa Simba amesema kuwa wanatambua wana kazi kubwa ya kufanya ili kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao ni muhimu kwao kupata pointi tatu.

“Utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani kwani wapinzani wetu wapo vizuri kiushindani hilo tunatambua nasi pia tupo vizuri.

“Kikubwa ambacho tunafanya ni kuwa tayari kwa ajili ya mchezo huo mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

Kwenye msimamo, Simba ipo nafasi ya kwanza ina pointi 61 ikiwa imecheza mechi 25 na Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27.

SOMA NA HII  USAJILI WA KWANZA WA MBRAZILI NDANI YA SIMBA HUU HAPA....ALIKUWA ANAKIPIGA ZNZ....