Home Simba SC WAAMUZI SIMBA V YANGA NI PASUA KICHWA KWA KWELI

WAAMUZI SIMBA V YANGA NI PASUA KICHWA KWA KWELI


 BAADA ya awali mchezo wa Ligi Kuu Bara kupangwa kuchezwa Mei 8, Uwanja wa Mkapa na waamuzi kupatikana  sasa imekuwa ni pasua kichwa kujua nani atakuwa mwamuzi watakapokutana Julai 3.

Awali kabla ya mchezo huo kuota mbawa, waamuzi ambao walipangwa ilikuwa ni pamoja na Emmanuel Mwandembwa aliyepewa jukumu la kuwa mwamuzi wa kati, Frank Komba aliyepangwa kuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Hamdani Saidi aliyepangwa kuwa mwamuzi namba mbili pamoja na Ramadhan Kayoko ambaye alipangwa kuwa mwamuzi wa akiba.

Baada ya mchezo huo kuyeyuka kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda kwa kueleza kuwa mabadiliko ya muda uliofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kutoka saa 11:00 jioni mpaka saa 1:00 usiku ni kinyume cha utaratibu wa kanuni. Jambo hilo lilifanya mchezo huo ughairishwe kwa kuwa timu zilitofautiana muda wa kwenda.

Yanga walipeleka timu uwanjani saa 10:20 na ilisepa saa 11:40 jioni na Simba ilipeleka timu saa 11:25 jioni jambo lililofanya ngoma isichezwe na kwa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania mchezo huo utachezwa saa 11:00 jioni, Julai 3.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Sud Abdi Mohamed amesema kuwa kwa sasa ni mapema kusema kama waamuzi hao watakuwepo kwenye mchezo ujao.

“Ni mapema kusema kama watabaki hao kwenye mchezo ujao maana lolote linaweza kutokea,”. 

SOMA NA HII  MGOSI AFUNGUKA A-Z NAMNA ANAVYOIPIGANIA SIMBA SC NYUMA YA PAZIA...