Home Yanga SC YANGA YAPEWA BEKI WA AS VITA

YANGA YAPEWA BEKI WA AS VITA




 BENCHI la ufundi la timu ya AS Vita ya DR
 Congo limebariki rasmi beki wa pembeni wa timu hiyo, Djuma Shabaan kujiunga na Yanga ikiwa tu watafikia kwenye makubaliano mazuri.

Beki huyo wa kimataifa wa DR Congo amekuwa katika kiwango bora, kiasi ambacho amezivutia timu nyingi ikiwemo Yanga ambayo inaelezwa wapo katika hatua nzuri ya kuweza kumnasa beki huyo ambaye amehusishwa na kutakiwa na Simba hivi karibuni.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha Msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu, amefichua kuwa kwa upande wao hawawezi kumzuia mchezaji yeyote kuondoka kwenye timu hiyo ikiwa atapewa maslahi mazuri, hivyo kama Yanga watatoa fedha watampata na litakuwa jambo zuri kwa mchezaji huyo.

“Kuhusu unachoniambia kwa upande wetu wala hatuna tatizo kama benchi la ufundi tupo tayari kumuachia.

“Unajua kwa upande wetu ligi ikishamalizika, tunatoa ruhusa kwa mchezaji yeyote kuondoka, sasa suala la Djuma ni hao Yanga wenyewe kufikia makubaliano na mchezaji ili aweze kujiunga nao, sisi hatuna shida kwa kuwa tuna kawaida ya kutengeneza wengine,” alisema.


SOMA NA HII  BINGWA MSIMU HUU KUPATIKANA MEI 24 AU JUNI 16...YANGA AKITELEZA TENA KIDOGO TU..SIMBA HUYOOO...