Home FA Cup YANGA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO,

YANGA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO,


 KIKOSI cha Yanga kimefanikiwa kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya ubao wa Uwanja wa Kambarage kusoma Mwadui 0-2 Yanga.

Mabao ya ushindi yote yalifungwa na kiraka Deus Kaseke dakika ya 24 na 56 na kuwafanya watinge moja kwa moja hatua ya nusu fainali.

Sasa watakutana na Biashara United ambayo ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa robo fainali uliochezwa jana, Mei 24, Uwanja wa Karume, Mara.

Kesho ni zamu ya mabingwa watetezi wa taji hilo Simba kusaka nafasi ya kushiriki nusu fainali ambapo itamenayna na Dodoma Jiji.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa ambapo utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  YANGA NA PACOME MPAKA AFCON