Home kimataifa AGUERO ANA KAZI KUBWA MBILI BARCELONA

AGUERO ANA KAZI KUBWA MBILI BARCELONA


SERGIO Aguero, nyota mpya wa Barcelona kazi yake ya kwanza kuifanya ni kuhakikisha kwamba anamshawishi staa mwenzake Lionel Messi kubaki ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo amejiunga na Barcelona akiwa mchezaji huru baada ya dili lake ndani ya Manchester City kumeguka na mabosi wa City ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England waliweka wazi kwamba hawatamuongeza kandarasi mpya.

Taarifa rasmi ambayo ilitolewa na Barcelona ilieleza kuwa nyota huyo ana kazi ya kumshawishi Messi abaki ndani ya timu hiyo kwa kuwa ni marafiki pia kuendeleza ubora wa timu hiyo ndani ya La Liga kwa kuwa ni moja ya timu kubwa duniani.


Pia Aguero mwenyewe ambaye ni mshikaji wa Messi wanacheza pamoja kwenye timu ya taifa ya Argentina jambo ambalo linaongeza nguvu kwa nyota huyo kuweza kumshawishi Messi abaki kwa kuwa mkataba wake unakaribia kuisha na hakuna taarifa kuhusu kuongeza kwake mkataba.

Aguero ambaye msimu wa 2021 haukuwa bora kwake ndani ya City kwa kuwa hakuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Pep Guardiola pia alishuhudia timu yake ikipoteza taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Chelsea, Jumamosi iliyopita.

“Yote kwa yote ana maamuzi yake ambayo anatakiwa kuyafanya na klabu, kwangu mimi itakuwa furaha tukicheza naye,” amesema Aguero. 

SOMA NA HII  GUARDIOLA HAITAKUWA KAZI NYEPESI MBELE YA PSG

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here