Home Yanga SC BAKARI MWAMNYETO AKIMBIZA KWA DAKIKA ZAKUTOSHA YANGA

BAKARI MWAMNYETO AKIMBIZA KWA DAKIKA ZAKUTOSHA YANGA


BAKARI Mwamnyeto, nahodha msaidizi wa kati msimu huu kwenye ligi akiwa Yanga amekimbiza jumla ya dakika 2,386 uwanjani.


Amecheza mechi 27 kati ya 31 akiwa amekosekana kwenye mechi 4 ambazo zimechezwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.


Kwenye msimamo ikiwa ya pili imefunga jumla ya mabao 49. Licha ya kwamba ni beki wa kati Mwamnyeto ametupia mabao matatu ambapo aliwafunga Ihefu, Gwambina na Mwadui FC.


Mechi 26 nyota huyo mzawa aliyeyusha dk zote 90 na mmoja alianzia benchi ilikuwa mbele ya Gwambina FC na alitumia dk 46.


Mechi alizoyeyusha dk zote 90 ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City , Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Polisi Tanzania, KMC, Biashara United, Simba, Namungo, Azam FC, JKT Tanzania, Ruvu Shooting. Mwadui , Dodoma, Ihefu, Prisons, Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar. Coastal Union, Polisi Tanzania, Namungo, JKT  Tanzania, Ruvu Shooting na Mwadui.


Mwamnyeto alisema kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zao zilizobaki ili kupata matokeo chanya.

SOMA NA HII  YANGA WAIPIGA MKWARA SIMBA KWA KUMUACHA MKUDE...ALLY KAMWE AFICHUA WALIYAHIFADHI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here