Home Yanga SC HUYU HAPA NYOTA KIBU ANAYETAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA

HUYU HAPA NYOTA KIBU ANAYETAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA


 IKIWA ni mchezo wake wa kwanza kucheza ndani ya timu ya taifa ya Tanzania, Kibu Dennis kwa sasa amekuwa gumzo kutokana na kutajwa kuingia rada za Yanga.

Weka kando ishu za nyota huyo kuhitajika Yanga ambapo yeye mwenyewe katika hilo alifunguka kwa kusema, ‘No Comment’ hapa Championi Jumatano inakuletea rekodi zake ndani ya Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Juni 13, aliweza kutoa pasi moja ya bao kwa nahodha John Bocco na kusababisha faulo iliyofungwa kiufundi na nyota Israel Mwenda.

Kibu alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni maelekezo ambayo alipewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen na kuweka wazi kwamba alifurahi kupata nafasi ya kulitumikia taifa la Tanzania mbele ya Malawi wakati ubao uliposoma Tanzania 2-0 Malawi.

Ikumbukwe kwamba Kibu aliibuka ndani ya Mbeya City zama zile ikinolewa na Kocha Mkuu, Amri Said akitokea Klabu ya Geita Gold ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Ameanza kikosi cha kwanza katika jumla ya mechi 21 ambazo ni sawa na dakika 1,890 amehusika kwenye mabao 7 kati ya 22 ambayo yamefungwa na timu hiyo.

Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 270. Kikosi hicho kinachonolewa na Mathias Lule kipo nafasi ya 14 na pointi zake ni 33 kinapambana kuweza kuona namna gani kinaweza kubaki ndani ya ligi.

Mechi zake za ugenini

Mechi 12 alianza kikosi cha kwanza ugenini ilikuwa mbele ya hizi hapa:-KMC, Uwanja wa Uhuru, Yanga Uwanja wa Mkapa, Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri, Mwadui, Uwanja wa Mwadui Complex.

 Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru, JKT Tanzania, Uwanja wa Samora, Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Biashara United, Uwanja wa Karume, Mara. Gwambina, Uwanja wa Gwambina Complex, Ihefu, Uwanja wa Highlands na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri.

 

Uwanja wa Sokoine

Uwanja wa nyumbani wa Mbeya City ni Uwanja wa Sokoine ambapo mechi ambazo alianza kikosi cha kwanza ni 9 ilikuwa namna hii:-Azam FC, Namungo FC,Tanzania Prisons, Simba, Ihefu, Polisi Tanzania,Kagera Sugar, JKT Tanzania, Ruvu Shooting.

SOMA NA HII  MUKOKO TONOMBE AVUNJA UKIMYA USAJILI YANGA....ADAI WALIKUWA WANAVUNJA TIMU BILA UTARATIBU...AFUNGUKA YOTE A-Z..

 

Mabao yake

Bao la kwanza aliwatungua Ihefu FC, Uwanja wa Sokoine dk 58, Polisi Tanzania, dk 6, Uwanja wa Sokoine, bao la tatu aliwatungua JKT Tanzania, Uwanja wa Samora, bao la nne Gwambina FC aliwatungua Uwanja wa Gwambina Complex kwa mkwaju wa penalti bao la tano alifunga mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Sokoine kwa kichwa  dk ya 18.

Pasi zake za mabao

Pasi mbili za mabao alitoa mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Sokoine dakika ya 45 na 67.

Eneo lake la hatari

Rekodi zinaonyesha kwamba Kibu ni hatari akiwa ndani ya 18 kwa sababu katika mabao 7 ambayo amehusika akiwa amefunga mabao matano na kutoa pasi mbili za mabao ni bao moja moja alitengeneza akiwa nje ya 18.

Mengine yote sita alitengeneza akiwa ndani ya 18 ambapo alifunga manne na kutoa pasi mbili za mabao. Ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Mbeya City.

Rekodi yake matata

Kibu anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee ambaye amefunga bao kwa kichwa akiwa nje ya 18 ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu wa 2020/21. Aliwatungua JKT Tanzania. Watupiaji wengine ambao wametupia mabao kwa kichwa ilikuwa ni ndani ya 18 kama ilivyo kwa Luis Miquissone ambaye aliwatungua Tanzania Prisons.