Home Yanga SC KUMBE CARLINHOS ALIPUUZIA PROGRAMU ALIYOPEWA NA MADAKTARI

KUMBE CARLINHOS ALIPUUZIA PROGRAMU ALIYOPEWA NA MADAKTARI


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa nyota wao Carlos Carlinhos aliomba kuondoka yeye mwenyewe jambo ambalo liliwafanya wamruhusu pia wameongeza kuwa hakuwa akifanya program aliyopewa na madaktari.

Jana Mei 31, Carlinhos alivunja mkataba na mabosi wake Yanga kwa makubaliano ya pade zote mbili baada ya kuzungumza.

Anasepa Yanga akiwa amecheza kwenye jumla ya mechi 15 katika mashindano yote ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa:”Ni kweli suala hilo limetokea ili klabu isiwe na mzigo na yeye awe na furaha kama ambavyo aliandika kwenye barua yake.

“Wakati timu ikiwa Shinyanga unajua yeye aliumia akiwa Ruangwa, madaktari walimuwekea programu ya kufanya ila hakuwa akifanya hivyo,” .

Nyota huyo ameshareja nchini kwake Angola akiwa amenyanyua taji moja ambalo ni Kombe la Mapinduzi na hakucheza hata mchezo mmoja Visiwani Zanzibar kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha.


SOMA NA HII  FT:- YANGA 1-3 APR.....SIMBA NJIA NYEUPEEE....SHIBOUB AKUMBUSHIA ENZI....SKUDU CHALII...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here