Home epl MBAPPE KUTUA LIVERPOOL

MBAPPE KUTUA LIVERPOOL


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool inaelezwa kuwa ana mpango wa kuimarisha kikosi chake na anahusishwa kuiwinda saini ya nyota wa PSG raia wa Ufaransa,  Kylian Mbappe. 

Mara kwa mara imekuwa ikielezwa kuwa Liverpool inahitaji saini ya Mbappe huenda dili likajibu baada ya staa huyo kusema kuwa anataka kuondoka.

Liverpool tayari imeshampoteza kiungo wao Georginho Wijnaldum ambaye ameibukia PSG hivyo nao wanataka kutumia mwanya huo kuinasa saini ya Mbappe.

Ripoti zinaeleza kuwa Liverpool ina nafasi kubwa ya kupata saini yake licha ya kwamba hata Real Madrid nao wanamhitaji nyota huyo.

SOMA NA HII  NABI ATOBOA SIRI KUBWA...MECHI DHIDI YA WAARABU...USHINDI MAPEMA TU!