Home news OSCAR OSCAR AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS TFF

OSCAR OSCAR AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS TFF


 LEO Juni 12, mchambuzi wa masuala ya michezo Tanzania na mtangazaji wa kituo cha E FM, Oscar Oscar, mzee wa Kaliua ametia timu makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Urais.

Oscar alichukua fomu hiyo Juni 10 baada ya kukamilisha utaratibu wa kutafuta wadhamini na kujaza fomu hiyo ameirejesha leo TFF.

Oscar ametinga makao makuu ya TFF na ndiga kali pamoja na msafara uliongozwa na bosi wake Majizo ambaye amemsindikiza kijana wake.

Anawania nafasi hiyo akiwa pamoja na Wallace Karia ambaye anatetea nafasi yake kwa mara nyingine kwa kuwa naye pia amechukua fomu. Mbali na Karia wengine ambao wanawania nafasi ya Urais ni pamoja na mchambuzi wa masuala ya michezo Ally Mayay.

Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba yupo pia Hawa Mniga abaye ni Mwanamke pekee aliyechukua fomu kuwania nafasi hiyo kubwa ndani ya TFF.

Zoezi la kuchukua fomu lilianza rasmi Juni 8 na leo Juni 12 inatarajiwa kuwa mwisho wa kuchukua fomu na kurudisha.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA SC WATUA KISHUA NIGERIA....RIVER UNITED WAPAGAWA...