Home Simba SC SIMBA YARUDISHA SHUKRANI KWA MASHABIKI

SIMBA YARUDISHA SHUKRANI KWA MASHABIKI


SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wachezaji wanastahili pongezi kwa ajili ya kupambana katika kutimiza majukumu bila kuwasahau mashabiki.


Jana, Juni 19 kikosi hicho kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
 
Bao la Simba lilifungwa na Luis Miqussone ambaye alipiga pigo huru akiwa nje ya 18 na kuipa pointi tatu Simba.
Matola amesema:”Wachezaji wanastahili pongezi kwa kuwa wanafanya kazi kubwa katika kusaka ushindi hivyo ni jambo jema na kubwa kwetu pamoja na mashabiki.
“Mashabiki nao ni watu muhimu kwa kuwa wamekuwa wakitupa sapoti hivyo ninapenda kuwaomba waendelee kuwa pamoja nasi bila kuchoka,” amesema Matola.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 70 baada ya kucheza jumla ya 28.
SOMA NA HII  ALICHOKISEMA ALLY MAYAI KUHUSU NANI BORA KATI YA PABLO NA NABI...AWATAJA FEI TOTO NA MORRISON...