TIMU ya Taifa ya Ufaransa imefungua pazia la Euro 2020 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani.
Katika mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo, kiungo Paul Pogba aloonyesha kiwango bora na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Ni Mats Hummels dakika ya 20 alijifunga na kufanya bao hilo kudumu mpaka dakika ya 90 ya mchezo katika Uwanja wa Allianz Arena.
Katika kundi F ni timu ya taifa ya Ureno inaongoza kundi ikiwa na pointi 3 na mabao matatu baada ya kushinda mbele ya Hungray.