Home Yanga SC YANGA WATAJA NAMNA WATAKAVYORUDI KIMATAIFA

YANGA WATAJA NAMNA WATAKAVYORUDI KIMATAIFA


INJINIA Hersi Said, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, amesema kuwa watarejea kimataifa kwa kupitia Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwa Simba.

Katika Kombe la Shirikisho, Yanga imetinga hatua ya nusu fainali ambapo inatarajia kucheza na Biashara United ikiwa watashinda hapo wanaweza kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Azam FC v Simba.

Injinia amesema:”Tutashiriki mashindano ya kimataifa bila kutegemea nafasi ya upendeleo na tutashiriki kupitia Kombe la Shirikisho, kumbuka kwamba tupo hatua ya nusu fainali na tuna amini kwamba tutashinda.

“Ikiwa tutachukua Kombe la Shirikisho basi hiyo itakuwa njia yetu kushiriki mashindano ya kimataifa. Kikubwa ni mashabiki kuendelea kutupa sapoti,” amesema.

Kwa upande wa Biashara United, kupitia kwa Ofisa Habari Idrisa Sechombo amesema kuwa kikosi chao kipo vizuri na wanaamini watapambana. 

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Biashara United ipo nafasi ya nne huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya pili.

SOMA NA HII  BAKARI MWAMNYETO AKIMBIZA KWA DAKIKA ZAKUTOSHA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here