Home Simba SC AL AHLY WAWEKA BILIONI NNE KUMVUTA LUIS MIQUISSONE MWENYEWE AKUBALI KUONDOKA SIMBA

AL AHLY WAWEKA BILIONI NNE KUMVUTA LUIS MIQUISSONE MWENYEWE AKUBALI KUONDOKA SIMBA


KAMA ulikuwa unahisi ni utani basi jua kuwa klabu ya Al Ahly wapo siriazi katika ishu ya usajili wa winga wa timu hiyo Luis Miquissone ambapo tayari klabu hiyo imewasilisha ofa ya pili ya Bilioni nne za Kitanzania kwa mchezaji huyo huku mwenyewe Miquissone akikubali kujiunga na Al Ahly.

Al Ahly kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa kuiwania saini ya Luis Miquissone mwenye uraia wa Msumbiji ambaye tangu ajiunge na Simba Januari 2020, amekuwa kwenye kiwango bora kinachozifanya klabu mbalimbali kumuwania.

Luis Miquissone ameonyesha kiwango bora katika michezo yote miwili ambayo simba ilicheza dhidi ya Al Ahly katika ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu uliopita ambapo alifanikiwa kuwafunga timu hiyo bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Wakala mmoja wa wachezaji kutoka katika kampuni ya FMC  inafanya kazi na Luis, ambaye jina lake hakutaka kutajwa amesema kuwa Al Ahly imetuma ofa ya Bilioni nne kwa Simba ambapo wiki hii wataanza kuijadili ofa hiyo kwa pande zote mbili, huku mchezaji mwenyewe akikubali kujiunga na Al Ahly baada ya kuuambia uongozi wake kuwa yupo tayari kujiunga na klabu hiyo.

“Klabu ya Al Ahly mara ya kwanza iliweka bilioni 1.6 ambazo zimeonekana kuwa ndogo kwa Simba lakini mara baada ya kutuma ofa ya bilioni nne kwa uongozi wa Simba, umeonekana kukubali kukaa mezani na Al Ahly kwa aajili ya mazungumzo ambapo wiki hii watakutanba kujadili ofa hiyo.

“Kuhusu mchezaji mwenyewe yupo tayari kujiunga na Al Ahly, tayari ameuambia uongozi wake kuwa yupo tayari kujiunga na kocha wake Pitso Mosimane ambaye walifanya kazi wote katika klabu ya Mamelodi Sundwons,” Kimesema Chanzo hiko.

Alipotafutwa mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu juu ya ishu hiyo amesema kuwa “Kila kitu kuhusu masuala ya usajili wa wachezaji wa Simba watakaoingia, na watakaotoka ipo chini ya Mtendaji mkuu wa timu ambaye anahusika katika kutoa taarifa hizo.

SOMA NA HII  FIFA KUTUA NCHINI KUIKAGUA SIMBA...ISHU YA AFRICAN SUPER CUP ...MCHONGO MZIMA UTAKUWA HIVI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here